Ahmed Ally awaomba radhi mashabiki Simba SC



Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally amewaomba radhi Mashabiki na Wanachama wa klabu hiyo, kufuatia kikosi chao kupoteza mchezo wa tatu wa Ligi Kuu msimu huu.

Simba SC jana Jumapili (Juni 26) ilipoteza mchezo wa Mzunguuko wa 29 katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, kwa kukubali kichapo cha 1-0 kutoka kwa wenyeji Tanzania Prisons, bao likifungwa na Nahodha Benjamin Asukile.

Mapema leo Jumatatu (Juni 27), Ahmed Ally ametumia kurasa zake za mitandao ya kijamii kuwataka radhi Mashabiki na Wanachama wa Simba SC, kwa kitendo cha kuangusha alama tatu ugenini.

Ahmed Ameandika: Hamkustahili maumivu mliyoyapata jana


 
January tulikuja hapa Sokoine tukawapa maumivu June tumerudi tena tumewapa tena maumivu makali

Mechi ya jana mlijua kabisa haitupi ubingwa lakini mlichotaka ni ushindi tuu ili tuendeleee kumwagilia moyo

Poleni sana msimu ujao sio mbali tutawafuta machungu,

Tutasahau magumu yote tuliyopitia msimu huu kicheko chetu hakiko mbali

Kwa sasa tuvumiliane tumalize msimu yajayo yanafurahisha,

Mwakani watakusanyikana vilevile kumwaga machozi

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad