Alikiba: Pesa Zinatosha Ndugu Zangu wa Kahama, Acheni Nipafomu Kwanza





Alikiba akiimba jukwaani Kahama mkoani Shinyanga
Staa wa Bongo Fleva, Alikiba usiku wa kuamkia leo amefanya bonge moja la shoo katika Mji wa Kahama mkoani Shinyanga katika sherehe ya kutimiza mwaka mmoja kwa kiwanja maarufu cha burudani katika mji huo cha The Magic 101.

Vibe la mashabiki kumtuza staa huyo lilikuwa kubwa kiasi cha mwenyewe kunyoosha mikono na kusema: “Pesa zimetosha ndugu zangu wa Kahama, acheni nipafomu.”

Licha ya Alikiba kuwataka mashabiki wasiendelee kumtuza, bado waliendelea kumiminika jukwaani na kumpa fedha pamoja na kupiga naye picha, wakionesha furaha waliyokuwa nayo kwa staa huyo kufanya shoo katika kiwanja hicho cha kipekee na cha kisasa cha burudani katika Mji wa Kahama

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad