Barbara Gonzalez Asimama Mguu Sawa na Kuwaambia Haya Mashabiki, Wanachama Simba SC Kuhusu Kinachoendelea



Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba SC Barbara Gonzalez amewataka Mashabiki na Wanachama wenye nia njema na klabu hiyo kutokuwa na wasiwasi katika kipindi hiki, ambacho baadhi yao wamedhamiria kuharibu taswira ya Msimbazi.

Siku chache baada ya Simba SC kupoteza mchezo wa Nusu Fainali Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ kwa kufungwa 1-0 na Young Africans, Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, baadhi ya viongozi wa zamani na waliopo madarakani wametoa shutuma kwa Muwekezaji na Afisa Mtendaji Mkuu kwa kudai ndio chanzo yaliyowafika.

Barbara amesema wanaofanya hivyo wana dhamira mbaya na Simba SC na walisubiri hali iwe kama ilivyo sasa ndipo waanze kusema mambo yasiyo na tija kwa kushinikiza baadhi ya viongozi kujiuzulu akiwemo yeye kama Afisa Mtendaji Mkuu.

“Kama kuandika barua na kuacha kazi hii ningefanya mwaka jana nikiwa mgeni katika soka, ila nilipiga moyo konde nilipambana na nikavuka wakati huo hadi kufika hapa,”


“Jambo hilo la kutokuwa na maelewano sio la kweli, kwani nimekuwa nikifanya nao kazi kwa maelewano makubwa na kupokea maelekezo kutoka kwao, sasa sijui haya mengine yanatokea wapi?”

“Shughuli zote za klabu kila siku zinakwenda chini yangu na nimekuwa nikifanya kila ambacho naagizwa kutoka kwa Mwenyekiti na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, kwani wao ndio mabosi zangu, lazima nifanye kazi vile wao wanahitaji.”

“Pia wapo wengine wamekuwa wakinishambulia na kusema mambo mengi, hawapo uongozini kwa sasa, lakini kwangu naona ni changamoto ya kuzidi kupambana kuhakikisha nafanya kazi kwa ufanisi zaidi ili kuhakikisha tunaifikisha Simba kwenye malengo iliyojiwekea,” alisema Barbara na kuongeza;


“Haya yote yanatokea kwa sababu Simba tumeshindwa kufikia malengo yetu ya kufika nusu fainali Kombe la Shirikisho Afrika, kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho (ASFC). Kama tungefanya vizuri na kufikia malengo ikiwemo kubeba mataji, haya yote yasingetokea.”

“Haiwezi tokea hata siku moja kutoa mbele na kuanza kujibu mambo mengine nayaacha yapite tu kama ilivyokuwa kama mengine ya huko nyuma akili na nguvu yangu nimeiweka kwenye mambo muhimu ya klabu,”.

“Siwezi kukatishwa tamaa au kuondoka kwenye malengo muhimu ya timu kuona jinsi gani msimu huu maeneo yapi yalitifanya tushindwe kuwa bora na kushindwa kufikia malengo ili kuboresha na kuwa kikosi imara msimu ujao kuchukua tena mataji.

“Mashabiki wa Simba wasiwe na wasiwasi viongozi tunafahamu changamoto msimu huu zilikuwa wapi tupo kwenye vikao muhimu vya ndani kuisuka tena timu upya katika maeneo muhimu na naimani tutarudi kwenye kiwango bora bila ya kujali mitihani tunayokutana nayo wakati huu.”

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad