Barbara "Simba SC Haijafeli Usajili, Tulieni Mtaona"

 


Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba SC Barbara Gonzalez amesema hadi sasa klabu hiyo imeshindwa kuipata saini ya mchezaji Victorien Adebayor aliyekua anaitumikia klabu ya USGN ya nchini Niger.


Simba SC ilijihusisha na usajili wa Mshambuliaji huyo, baada ya kuridhishwa na uwezo wake aliouonesha kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika msimu wa 2021/22.


Barbara amesema hadi sasa Simba SC haijafeli katika usajili wa mchezaji yoyote waliyemdhamiria kwa msimu ujao wa Ligi Kuu na Michuano ya Kimataifa, zaidi ya Adebayor anayedaiwa kutua kwa Mabingwa wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika RS Berkane.


“Kumekua na taarifa nyingi kuwa tumeshindwa kuwasajili wachezaji kadhaa, sio kweli hata kidogo, tunakiri kumkosa Adebayor pekee yake, lakini kwa wengine ambao tumewadhamia tupo katika hatua nzuri za kuwasajili na watacheza Simba SC msimu ujao.”


“Simba SC inatajwa sana kwa sababu mawakala wengi wanaitumia klabu yetu kuwapandisha thamani wachezaji wao, lakini nikwambie tu tupo makini na tumeshalifahamu hilo, tunasajili kimya kimya.”


“Muda utakapofika tutawatangaza wachezaji tuliowasajili kwa ajili ya klabu yetu, Mashabiki na Wanachama waendelee kuwa watulivu, Uongozi wao upo kazini na utakamilisha kila hatua iliyoidhamiria katika usajili.” Amesema Barbara.


Simba SC imedhamiria kufanya usajili mkubwa kwa ajili ya kukiboresha kikosi chao kwa msimu ujao wa Ligi Kuu na Michuano ya Kimataifa, baada ya kushindwa kufikia lengo msimu huu 2021/22, huku ikipoteza mataji yote ya Tanzania Bara.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad