Jana Jumanne (Juni 28) Simba SC imemtambulisha Zoran Maki raia wa ureno kwa mkataba wa mwaka mmoja ambaye amekuja kuchukuwa nafasi ya Pablo Franco alie ondoshwa klabuni hapo kwa kushindwa kufikia malengo alio pewa na Viongozi wa Simba
Zoran Maki akiwa kocha wa Simba SC anatakiwa kuchukuwa ubingwa wa NBC Premier league na kuifikisha timu nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika ndiyo malengo aliyo wekewa na uongozi wa Simba
Lakini Je! Viongozi wametimiza Mambo ya kuweza kufanikisha kocha kutimiza malengo hayo walio mpatia tena kwa mwaka mmoja ambao ni muda mfupi sana leo hii Klabu kama Real Madrid, Al Ahly, Manchester United zinafukuza makocha kwa sababu Viongozi wanatimiza majukumu yao kwa kumpatia kila kitu kocha ndy maana wanawafukuza
Viongozi wa Simba SC wanatakiwa kufanya sajili Bora za wachezaji, Preseason Bora, Kambi Bora ya wachezaji, Benchi zuri la Ufundi na kumpa ushirikiano mzuri kocha ili aweze kufanikisha malengo walio muwekea na sio kusubiri maajabu
NB: Usajili mzuri wa wachezaji ni muhimu
✍🏽Fredy John Jr.