CCM Yaruhusu Wanachama Kujiunga na Chama Chochote Cha Siasa


Katibu wa Itikadi na Uenezi @shakazulu36 , amesema kwa mujibu wa katiba ya nchi watanzania wana haki na uhuru wa kuchagua chama chochote cha siasa na kujiunga nacho.


Amesema hayo kwenye mkutano uliofabyika kwenye tawi la CCM Likunja, kata ya Likunja wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi ambako alipokea zaidi ya wanachama 50 kutoka vyama vya upinzani.


“Tuko kwenye maridhiano ya kisiasa ya kufanya siasa safi, siasa za maendeleo na kila mtu yuko huru kwenda Chama chochote anachoona kinamfaa kufanya siasa na kushiriki maendeleo ya nchi yetu. Niliuliza mara mbili mbili je! hawa wanakuja ccm kwa hiayari yao? nikaambiwa wameamua wenyewe, nami nawakaribisha sana mmefanya uamuzi wa busara”.


Wanachama hao kutoka vyama vya Chadema ,ACT wazalendo na CUF walimkabidhi Shaka, kadi, bendera, sare, hotuba za wenyeviti wao, na katiba za vyama hivyo.


Akiwa katika siku yake ya mwisho ya ziara ya mkoa wa Lindi, Shaka ametoa maelekezo kwa mkuu wa wilaya pamoja na mwenyekiti wa CCM, wilaya ya Ruangwa kwenda kijiji cha Likunja kuchunguza tuhuma za ufisadi na wizi zinazowakabili viongozi wa eneo hilo.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad