Corazon alisema urafiki hauwezi kuisha kwa sababu wamefahamiana kwa muda mrefu sana
Corazon alisema urafiki hauwezi kuisha kwa sababu wamefahamiana kwa muda mrefu sana
Corazon Kwamboka hatimaye amejitokeza wazi kufichua umma kwamba yeye na Frankie hawako pamoja tena kama wapenzi.
Akiwa kwenye mahojiano na MUngai Eve alisema waliamua kuachana kwa sababu mambo hayakuenda sawa na walivyotarajia na walisema ni sawa waachane.
Hata hivyo Corazon alisema kuwa wao ni wazazi pamoja, na kuongeza kuwa Frankie ni rafiki yake mkubwa na ikiwa ana suala huwa anamwambia na huwa wanakuwa pamoja mara nyingi lakini si wapenzi bali marafiki wenye faida.
Corazon alisema urafiki hauwezi kuisha kwa sababu wamefahamiana kwa muda mrefu sana.
"Mambo yalbadilika sana maishani mwangu baada ya kuachana na Frankie hi ni baada ya kubarikiwa na mtoto wetu wa pili,licha ya kuachana sisi ni marafiki, uhusiano wetu ulianza kama marafiki, na tulijuana kitambo sana
Nikiwa na jambo la kuzungumza na Frankie huwa tunazungumza, na kulea watoto wetu pampja, somo muhimu ambalo nimejifunza kwa hili ni vyema wazazi wazungumze na wawasiliane wanapowalea watoto wao."
Huku akifichua uhusiano wake na Vera Sidika, mwanasosholaiti huyo alisema kwamba Vera alimpa block, ingawa hawakuwa wanajuana sana.
Sababu ya kumpa block alisema kwamba haijui.
Pia akijibu mtindo wa kuiga Vera alisema kwamba ikiwa ana pesa kwa nini asimsherehekee bintiye. Na ikiwa watu hawana njia ya kusherehekea watoto wao ni juu yao.
Alisema kuwa watu hao wanaodai kuwa aliiga Vera wana uchungu na maisha yao