Daraja la Wami Kuanza Kutumika Mwezi wa Saba






Serikali imesema ujenzi wa Daraja jipya la Wami lenye urefu wa mita 513.5 na barabara za maingilio (km 3.8), unatarajiwa kuandika historia mpya kwa sekta ya Ujenzi mradi kukamilika kabla ya muda uliopangwa kwenye mkataba.
Ujenzi huu ulioanza mwezi Oktoba, 2018 unatarajiwa kukamilika mapema ifikapo mwezi Julai, 2022 badala ya mwezi Novemba kama ilivyo kwa mujibu wa mkataba wake. Hayo yamesemwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof.

Makame Mbarawa, wakati akishuhudia ukamilikaji wa sehemu ya kupita magari (deck) kwenye daraja hilo jipya ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 77.

Ujenzi wa Daraja Jipya la Wami una lengo la kutatua changamoto zilizokuwepo katika Daraja la zamani kutokana na kutokidhi mahitaji ya watumiaji wa daraja hilo tangu lilipojengwa Mwaka 1959. #globalpublishers #globalpublishersupdates

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad