Diarra, MANULA na Metacha Waongoza Clean Sheets Ligi Kuu Bara


Diarra, anaongoza kwa kucheza mechi nyingi bila kuruhusu bao 'clean sheets', kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara inayoelekea ukingoni, huku makipa watatu, Metacha Mnata wa Polisi Tanzania, Aboubakar Abbas wa Coastal Union na Hamad Kadedi wa Mbeya Kwanza wakiongoza ...

kwa kuokoa mikwaju ya penalti.

Diarra, mpaka kufikia raundi ya 26 ya Ligi Kuu, timu zikibakisha mechi tano na zingine nne kumaliza ligi, ana 'clean sheets' 15 na kwa upande mwingine Metacha Mnata anaongoza kwa kuokoa penalti mbili mpaka sasa, akiwa kipa pekee aliyeokoa nyingi kuliko wengine.

Kwa mujibu wa takwimu za Ligi Kuu, kipa wa Simba, Aishi Manula anashika nafasi ya pili kwa 'clean sheets' nyuma ya Diarra akiwa nazo 11, kipa mwingine wa Yanga, Abdallah Mshery yeye akiwa nazo tisa, zingine akiwa ametoka nazo kwenye klabu yake ya zamani, Mtibwa Sugar, kabla ya kujiunga na timu hiyo kipindi cha dirisha dogo.

James Ssetuba wa Biashara United na Metacha wa Polisi Tanzania wao wamekaa golini mechi nane bila kuruhusu wavu wao kuguswa kila mmoja, kipa wa Mbeya Kwanza, Hamad Kadedi na Said Kipao wa Kagera Sugar wakiwa wana 'clean sheets' saba kila mmoja.

Metacha, Kadedi na Aboubakar wanaongoza kwa kuokoa penalti mbili kila mmoja, Ahmed Salula wa Azam FC, Mshery wa Yanga, Ssetuba wa Biashara United, na Mohamed Makaka wa Ruvu Shooting kila mmoja ameokoa penalti moja.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad