Ni headlines za chupa la “I miss You” la Kwake Vivanny Boy @rayvanny kutokana na kile alicho kisema baada ya chupa hilo kutoka,kubwa ni kuwa anakuwa msanii wa kwanza Tanzania na Afrika Mashariki kiujumla kujenga nyumba na kuichoma kwenye shooting ili tu aweke uhalisia kwenye video yake, lakini pia Vanny Boy anaamini Uwenda Chupa hilo ndilo likawa chupa lililotumia mkwanja mrefu hadi kukamilika kwake, kuliko vyupa vyote Bongo.
Hasa kwenye Tambo la U-Heard na @soudybrown hii leo June 3, @directorivan_ ambaye ndiye aliyepewa dhamana ya kuongoza chupa hilo, amedai si, bali ni zaidi ya milioni 85 zilizotumika hadi “I miss You” inakamilika,lakini pia ni gharama kubwa zimetumika kwenye scene ya Helicopter,maana shots nyingi ilibidi zirudiwe baada ya muhusika kutaka iwe hivyo,na kwa nusu saa tu,hela ndefu ilikuwa ikilipwa.
Ivan pia amedai kwa upande wa nyumba, si ya maboksi kama wengi wanavyo sema,ni nyumba za mbao kama zile za kimarekani, na ili nyumba iliyokusudiwa ipatikane, Kulifanyika ujenzi kama mara tatu,ilibomolewa pale ilipoonekana haijakaa sawa na kujengwa upya