DPP amuachia huru Kisena, Mkewe na wengine watatu


michuzijr.blogspot.com
3h


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru aliyekuwa Mkurugenzi wa Mradi wa Mabasi yaendayo kasi, Dar es Salaam (UDART), Robert Kisena, mke wake, Frolencia Mashauri na wenzao watatu baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kuwasilisha Nolle kuwa hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi yao.

Washtakiwa walikuwa wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi.

Hata hivyo, Mahakama imewaamuru upande wa Jamuhuri kama watakuwa na nia ya kuwashtaki tena washtakiwakwa makosa hayo basi wasiwakamate hadi pale upelelezi ukikamilika.

Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Rita Tarimo ametoa amri hiyo leo Juni 3, 2022 baada ya Wakili wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Pendo Temu kuwasilisha Nolle Proseque kuwa DPP hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya washtakiwa.


 
"Mahakama inakubaliana na nia ya DPP kwa hiyo inawaachia huru washitakiwa wote, lakini kama mnataka kuwashtaki tena kwa makosa haya haya, basi msiwakamate tena hadi upelelezi ukamilike,"amesema Tarimo.

Mbali na Kisena na Florencia washtakiwa wengine ni Kulwa Kisena, Charles Newe na Chen Shi.

Hata hivyo, Kisena na Kulwa wao hawakuweza kwenda nyumbani kwa sababu wanakabiliwa na kesi nyingine ya uhujumu uchumi ambayo ndani yake ina mashtaka yasiyokuwa na dhamana.


Kesi iliyoondolewa leo na DPP imekaa miaka mitatu bila upelelezi kukamilika. Washitakiwa hao walikuwa wanatetewa na Wakilii Nehemiah Nkoko.

Katika kesi hiyo, Kisena na wenzake wakikuwa wanakabiliwa na mashitaka 15 kati ya 19 ikiwamo kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kuisababishia Udart hasara ya Sh 2,414,326,260.70.

Inadaiwa kuwa kati ya Oktoba 2012 hadi Mei 31, 2018 washtakiwa wanadaiwa kutenda makosa hayo.

Inadaiwa kati ya Januari Mosi, 2011 na Mei 31,2018 katika mahali tofauti wakiwa na watu wengine waliratibu shughuli za kiharifu huku wakijua kufanya hivyo ni kosa la kisheria.


 
Inadaiwa kati ya Januari Mosi ,2015 na Desemba 31,2017 katika eneo la Jangwani washtakiwa hao wakiwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Zenon Oil Gas Limited alijenga kituo cha mafuta kinachoitwa. Zenon Oil and Gas katika karakana ya Kampuni ya Udart bila ya kuwa na kibali kutoka Mamlaka ya Uthibiti wa Huduma na Nishati na Maji(Ewura).
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad