Dr. Mwigulu " Mtanzania Anayefikisha umri wa Miaka Kumi na Nane Anatakiwa Kulipa Kodi"



Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Mwigulu Nchemba amesema Serikali inakusudia kutoa namba ya utambulisho wa Mlipa Kodi (TIN) kwa kila Mtanzania atayefikisha umri wa miaka kumi na nane kwani atatakiwa kuanza kulipa kodi katika umri huo.


Dr. Mwigulu ameyasema haya leo wakati akiwasilisha Bungeni Dodoma mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2022/2023 huku akinukuliwa akisema "Kila Mtanzania mwenye umri wa zaidi ya miaka 18 na mwenye kipato anatakiwa kulipa kodi ambapo ili kutimiza amza hiyo Serikali inakusudia kutoa namba ya utambulisho wa mlipakodi (TIN) kwa kila mtanzania mwenye umri wa kuanzia miaka 18 au zaidi"


"Kwakuwa utaratibu wa usajili wa namba ya utambulisho wa Taifa (NIDA) unamtaka kila mwananchi mwenye umri wa miaka 18 au zaidi kujisajili NIDA, napendekeza kuwa wale wote wenye NIDA kwa sasa (wanaofikia milioni 19 nchi nzima) wapatiwe namba ya TIN na itumike kwenye miamala yote inayofanyika katika ununuzi na mauzo yanayofanyika ndani ya nchi ambapo kila mwenye namba ya mlipakodi atapata makadirio yake kwa njia ya simu na kulipa kodi husika kwa njia ya mtandao"

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad