G7 yaahidi msaada wa kifedha kukabiliana na mgogoro wa chakula duniani

 


Kundi la mataifa saba yaliyostawi zaidi kiviwanda duniani G7 linatarajiwa kuhitimisha mkutano wake wa kilele leo Jumanne kwa kutoa ahadi ya kifedha kuelekea juhudi za kukabiliana na mgogoro wa chakula duniani uliochochewa na vita vya nchini Ukraine. 

Viongozi wa Uingereza, Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japan na Marekani wanapanga kutoa tamko la pamoja juu ya maendeleo yaliyopatikana katika mkutano huo uliofanyika katika hoteli ya Schloss Elmau hapa Ujerumani. 


Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, ambaye ni mwenyeji wa mkutano huo mwaka huu, anatarajiwa kuandaa mkutano na waandishi wa habari baadaye hii leo. 


Viongozi hao wa G7 pia wametoa ishara ya mshikamano dhidi ya Urusi ikiwemo kupunguza utegemezi wa nishati kutoka Moscow, na kuiwekea nchi hiyo vikwazo pamoja na kuiunga mkono Ukraine katika vita vyake dhidi ya Urusi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad