HARAKATI za uchaguzi mkuu wa klabu ya Yanga zimeanza kushika kasi, mara baada ya wanachama mbalimbali kujitokeza katika zoezi hilo, huku upande wa wadhamni na wafadhili wa tiomu hiyo kwa sasa, kampuni ya GSM ukionekana kuwa na nguvu huku idadi kubwa ya watu wao na marafiki zao wakionekana kujitosa kwenye kinyang’anyiro hiko. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)
Uchaguzi wa klabu hiyo utafanyika Julai 10 mwaka huu, kwa nafasi za Urais, makamu wa rais sambamba na wajumbe watano watakaochaguliwa na mkutano mkuu.
Mpaka sasa katika nafasi ya rais, aliyejitokeza ni mkurugenzi wa uwekezaji wa kampuni ya GSM, na makamu mwenyekiti wa kamati ya mashindano wa klabu hiyo Mhandisi Hersi Said ambaye anaonekana kuwa mmoja ya mgombea mwenye nguvu kwenye nafasi hiyo mpaka sasa.
Hersi alichukua fomu kimya kimya siku za hivi karibuni mara baada ya utaratibu huo kutangazwa na Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya klabu hiyo Wakili Mchungahela, na siku ya jana Juni 9 alirejesha fomu hiyo huku akisindikizwa na baadhi ya wanachama wa klabu hiyo.
Mmmoja ya wanachama aliyemuunga mkono mtia nia huyo, ni makamu Mwenyekiti wa sasa ambaye anamaliza muda wake kwenye uongozi huo, Fredrick Mwakalebela, ambapo siku ya jana mbele ya wanahabari aliweka wazi msimamo wake wa kutoendelea kwenye cheo hiko, na hivyo ataamunga mkono Hersi Said kwenye nafasi ya urais.
“Mimi dhamira yangu haikuwa kuchukua fomu kwa msimu huu, tumeona jinsi tulivyopipokea timu katika kipindi kigumu na tumefika kipindi cha neema, hatuwezi kusema tumefika hapa peke yetu, kuna watu walikuwa nyuma kusaidia kufika pale.” Alisema Mwakalebela
Yanga inakwenda kufanya uchaguzi huo kwa mara ya kwanza, toka walipofanya mabadiliko ya katiba na hivyo cheo cha Mwenyekiti wa klabu hiyo kwa sasa nkitfahamika kama rais wa klabu.
Aidha kiongozi huyo mwandamizi aliendelea kusema kuwa, aliamua kuja klabuni hapo siku ya jana, ili kuwaaga rasmi wanachama na mashabiki wa timu hiyo kwa kuwa hatogombea tena kwenye uchaguzi huu, bali kwa sasa ataunga mkono jitihada za mhandisi Hersi Said ambayo amerudisha fomu ya nafasi ya urais.
“Mimi nimekuja kuaaga rasmi mashabki wa Yanga kwamba sitagombea na kuUnga mkono jitihada za Hersi kugombea urais kwa klabu yetu ya Yanga.” Alisitiza kiongozi huyo
Mpaka kufikia siku ya jana jioni, kwenye nafasi ya urais ni Mhandisi Hersi pekee ndio aliyerudisha fomu hiyo, huku ikielezwa baadhi ya wanachama kama Davis Mosha naye mwenyekiti wa zamani wa klabu hiyo kuwa nae amejitosa kwenye kinyang’anyiro hiko.
Licha ya Mwakalebela kuachia nafasi hiyo, lakini imegundulika kuwa huwenda nafasi ya makamu rais ndani ya klabu hiyo, tayari imeoneshewa nia na Arafat Mohamed ambaye ni mjumbe wa kamati ya utendaji wa Yanga na mkurugezni wa Shirika la Bima Zanzibar.
Arafat ni moja ya watu wa karibu wa kampuni ya GSM ambao ni wafadhiri na wadhamini wa klabu hiyo.