Haijawai Kutokea Yanga Yatikisa Jiji, Msafara Wao, Basi Lageuka Kivutio






HAIJAWAHI kutokea unaambiwa. Hiyo ni mara baada ya Yanga kufunga mitaa ya Jiji la Dar es Salaam na kujaa jezi za kijani na njano wakati wakilitembeza kombe lao la ligi kuu ambalo wamelibeba msimu huu.


Yanga ambao walitua jijini Dar majira ya saa tano asubuhi wakitokea jijini Mbeya ambako walitoka kucheza na Mbeya City juzi Jumamosi na kukabidhiwa kombe lao, walikaribishwa na mashabiki lukuki ambao walijitokeza kwa wingi kuipokea timu yao.

Championi Jumatatu lilishuhudia historia ya wingi wa mashabiki wa Yanga ambao pengine haujawahi kuonyeshwa na mashabiki wa timu nyingine kutokana na kuusindikiza msafara wa timu kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), mwanzoni wa safari mpaka mwisho.




BASI LAGEUKA KIVUTIO
Aidha, kwa upande mwingine, basi la wazi ambalo liliwabeba wachezaji wa Yanga, viongozi na makocha, liligeuka kuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki wa Yanga ambao walikuwa wakilishangilia.

Basi hilo ni aina ya mabasi ambayo yamekuwa yakitumiwa na timu kama za Ulaya ambazo hutumia kutembeza ubingwa wao mara baada ya kubeba makombe, Yanga wamekuwa wa kwanza kulitumia basi hilo kwa Tanzania.


 

YANGA YALINYANYUA KOMBE MSIMBAZI

Katika hatua nyingine, Yanga waliamua kulinyanyua kombe lao katika makao makuu ya Klabu ya Simba na kusimama kwa muda kisha kulinyanyua kombe hilo.

Katika kuhakikisha Yanga inawakera zaidi Simba, waliamua kulinyanyua kombe hilo kupitia msemaji wa timu hiyo, Haji Manara.

Hata hivyo, mashabiki wa Simba pia walijibu mapigo kwa kunyoosha bendera zao za Simba juu ya jengo hilo na kuwajibu mapigo Yanga ambao walipita zao na kuelekea Jangwani.



MAYELE ATETEMA JANGWANI

Wakati Yanga wakiwa katika utambulisho wa mchezaji mmojammoja walipotua katika makao makuu ya Yanga Jangwani, Fiston Mayele aliamua kutetema wakati alipotambulishwa kuja kuwapungia mkono mashabiki wa timu hiyo waliojaza Jangwani yote na kuamsha shangwe la maana.


SHEREHE ZAHAMIA GSM

Baaada ya kupita Jangwani kwa utambulisho wa wachezaji na benchi la ufundi la Yanga, msafara ulihamia katika makao makuu ya Kampuni ya GSM, Sara Saramander Tower Posta ambapo sherehe zilihamia hapo kwa wasanii mbalimbali kutumbuiza.

Stori na Marco Mzumbe



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad