Leo ni siku ya maadhimisho ya watu wenye ulemavu wa ngozi, Msemaji wa club ya Yanga @hajimanara ametumia ukurasa wake wa Instagram kuwataka watu hao wasijisikie vibaya na kujivunia kwakuwa wana uwezo wa kufanya mambo makubwa zaidi.
"Ujumbe wangu kwa rafiki zangu wenye Ualbino.
"Leo ni siku ya kimataifa ya watu wenye Albinism duniani na mimi kama mtu mwenye Ualbino, naungana na Jumuiya ya Kimataifa kuwatakia kheri nyingi wenzangu wote kote ulimwenguni 🙏🏻
Najua sio rahisi kutoboa kwa baadhi ya watu, hususan wenye mila potofu na imani haba hasa huku Afrika, lakini inawezekana.
Unaweza kufanya lolote lile pengine kuliko linalowezwa kufanywa na binadamu wengine, ikiwa una malengo sahihi, binafsi napitia changamoto nyingi za kubezwa kwa rangi yangu lakini sijawahi kurudi nyuma.
"Unaweza kuwa msomi, unaweza kuwa tajiri, unaweza kuwa mwanasiasa, unaweza kuwa mwanamuziki ,unaweza kuwa daktari ,,na hata kuwa maarufu na mashuhuri kweli kweli kama nilivyo mimi hii leo, licha ya Ualbino wangu.
Usijisikie vibaya hata kidogo na jivunie ulivyo na mshukuru Muumba wako, wewe ni sehemu ya matakwa ya Mungu aliyeahidi katika vitabu vyake kwamba, atawaumba wanadaamu vile atakavyo yeye.
Endelea kutumia karama zozote alizokujaalia Mungu wako kuionyesha jamii kwamba YOU CAN.
Ona kaka yako Bugati, naishi katika kundi la wafuasi wa mpira wenye ushindani mwingi na baadhi yao ambao si wastaarabu, huja na dhihaka na matusi ya kila namna kwa sababu mimi ni Albino, nini? nasonga mbele na namuangalia anaekutukana najiona nimemzidi kila kitu, kuanzia pesa, jina kubwa, umashuhuri, wake wazuri na hata kuishi tu maisha ya nyumbani, anakukejeli ukimwangalia vema unaweza kumuajiri kwako kupeleka watoto shule au kusafisha mabanda ya kuku uani.
"Yes, msikubali kuwa wanyonge hata siku moja kwa jinsi ulivyo Inshaallah Mungu atawalinda na kuwasaidia sababu yeye ndio kataka iwe hivyo, Mjivunie kwake vile alivyowaumba.
Leo katika football ya Tanzania hayupo yeyote anaenizidi kwa mikataba ya kibiashara ya matangazo na haipo Club wala mtu binafsi aliyepo direct kwenye football anaenisogelea huku mitandaoni kwa followers na kufuatiliwa licha ya Ualbino wangu,