Harmonize akashifiwa kwa kuvalisha Kajala Pete



Harmonize na Kajala
Bw. Pimbi kutoka Bongo amekosoa  Harmonize kwa kuvalisha  Kajala Pete, akihojiwa na Mbengo Tv  alidai kuwa kitendo hicho haikuwa na usawa.

''Naona maluweluwe, Kajala ni mke wa mtu, na huyu mlasigara bwege ni mume wa mtu'' Pimbi alisema.


 
Alisema ni kinyume cha sheria kuoa mke au mume wa mtu ikiwa hawajaachana rasmi,na hilo lilikuwa jambo la aibu.

''Kajala ni mke wa mtu na huyo mlasigara bwege ni mume wa mtu, hajatangaza kumpa talaka aliyemuacha  yule ,Mtaliano, na huyu mwingine mume wake hajatangaza kumpa talaka wala kumuacha, sasa wewe uoni kama mwanandoa ,mwanandoa amefunga ndoa kesi hiyo'' Pimbi alisema

Aliongeza kwa kusema kuwa wawili hao wanaweza kushtakiwa kwa kuvunja ndoa ya wapenzi wao wa zamani.


''Mkifunga ndoa,mnafunga kwa mkataba,mkiachana inabidi muachane kwa ukataba,hawajawachana kwa mkataba, wameachana kwa maneno ya mdomo, kwa hiyo ata kwa Mungu, ama ukienda kwa Serikali bado inatambua ndoa ya wapenzi wao wa  zamani'' Pimbi alisema.

Pimbi pia alidai kuwa, hili kufika kwa ndoa kuna hatua kadha na kuvalishana Pete ni mojawapo,hiyo inadhihirisha wazi kuwa tayari mnaelekea kwa ndoa.

''Mume wa mtu anakuvalishaje Pete, na  wewe mke wa mtu unakubali kuvalishwa Pete kivipi na mume wa mtu na unandoa yako, na talaka hauna ni tabia mbaya'' Pimbi alisema.

Pimbi alikanusha madai ya watu kusema kwamba ako na wivu dhidi ya wawili hao kuvalishana Pete.


 
''Kwa nini nikuwe na chuki na wewe na umeoa Bikizee, oa mtoto mbichi alafu nitakuonea wivu, kwamba kaoa katoto kali,umeoa ajuza, Bikizee mwenye mwaka arubanne na tano, ili uitwe mzee ni kuanzia miaka arubanne na tano'' aliongezea.

Harmonize alivalisha Kajala Pete siku ya Jumamosi wakati wa hafla ya jioni ya chakula cha mchana ambapo walikuwa wamewaalika wageni kushuhudia tukio kuu la uhusiano wao.

''Tumekuwa marafiki kwa takriban miaka saba, sidhani kama kuna mtu anajua hilo [Sidhani kama kuna yeyote kati yenu anayejua hili]. Tulianza kama marafiki, watu ambao wanafahamiana...” Harmonize alianza, akimtaja Kajala kuwa ni rafiki yake mkubwa na mpenzi wa maisha yake.

Aliendelea kufafanua kuwa urafiki wao ulikuwa wa uhusiano mzuri, akibainisha kuwa hakufikiria kuwa Frida angemkubali baada ya kuachana kwao.


Akizungumza baada ya kukubali pendekezo hilo kutoka kwa Harmonize, Kajala aliweka wasi kuwa changamoto walizokutana nazo pamoja hadharani na faraghani  ni sehemu ya maisha.

Frida pia alidai  kuwa angependa harusi  yao ifuate katika miezi miwili zijayo.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad