Mamlaka ya Ubelgiji imekabidhi jino la Kiongozi wa Uhuru wa Congo Patrice Lumumba kwa Familia yake katika hafla iliyofanyika Brussels.
Jino hilo nii sehemu pekee ya mabaki ya mwili wake ambayo inadhaniwa kuwa bado ipo baada ya kunyongwa na kisha mwili wake kuyeyushwa kwa tindikali mnamo 1961.
Ubelgiji ilikuwa mamlaka ya zamani ya kikoloni na uchunguzi rasmi ulisema kwamba baadhi ya wanachama wa serikali yake wakati huo waliwajibika kimaadili kwa hali iliyosababisha kifo.
Polisi wa Ubelgiji Gerard Soete, aliyesimamia kuharibiwa kwa mwili huo, alichukua jino hilo kama aina ya nyara ya uwindaji.
François Lumumba, Mtoto mkubwa wa Waziri Mkuu huyo wa zamani anasema Familia inataka zaidi ambapo kwa msaada wa Mawakili wake, anaiomba Serikali ya Ubelgiji kutoa maelezo ya kina kuhusu kifo cha Baba yao na kurejesha nyaraka zote zinazohusiana na kifo chake “Maombolezo yetu hayataisha kwa kurejeshwa kwa mabaki ya Baba yetu, tunataka kujua ukweli wote kuhusu kifo chake na wahalifu ambao bado wako hai waadhibiwe”