Klabu ya Manchester United ya England imethibitisha kuwa kiungo kutoka nchini Ufaransa Paul Labile Pogba ataondoka klabuni hapo mwishoni mwezi Juni, kufuatia kutamatika kwa mkataba wake.
Kiungo huyo raia wa Ufaransa ataondoka klabuni hapo, baada ya kugoma kusaini mkataba mpya, wakati wa msimu wa 2021/22 uliomalizika majuma mawili yaliyopita, huku Manchester United ikishika nafasi ya 6 kwenye msimamo wa Ligi ya England.
Uongozi wa klabu hiyo uliweka dhamira ya kumbakisha Pogba, lakini maamuzi yake ya kugoma kusaini mkataba mpya yalisitisha mpango huo, na sasa wameanza kumsaka mbadala wake kuelekea msimu ujao 2022/23.
Pogba aliyerejeshwa Manchester United kwa ada ya uhamisho ya Euro milioni 100 kutoka Juventus, na tetesi zinaeleza kuwa anaondoka tena klabuni hapo huku Juventus ikiwa kwenye hatua nzuri kumrejesha.
Aliporejea klabuni hapo mwaka 2016 hadi leo inathibitika ataondoka, kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29 amecheza michezo 154 na kufunga mabao 29.
Novak Djokovic chali French Open
Pogba alianza kucheza Soka Machester United katika kikosi cha vijana kati yam waka 2011– 2012 na baadae alipandishwa kikosi cha kwanza, ambapo alicheza michezo mitatu katika msimu wa 2011–2012.
Mwaka 2012 aliondoka klabuni hapo na kujiunga na Juventus ya Italia, ambayo aliitumikia katika michezo 124 na kufunga mabao 28.