Haya ndio mashtaka mapya ya Sabaya na wenzake



Aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro Lengai Ole Sabaya na wenzake watatu wamefikishwa kwa mara ya kwanza mahakama ya hakimu mkazi Moshi kwa tuhuma ya kesi ya kosa namba mbili ya uhujumu uchumi ya mwaka 2022 yenye mashtaka saba akiwa yeye na wenzake wanne 
Akisoma hati ya mashtaka wakili wa serikali Tumaini Kweka akiwa na mawakili watatu wa serikali amewataja watuhumiwa watano ambapo mtuhumiwa wa kwanza ni aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya,mtuhumiwa wa pili ni Silvester  Wenceslaus Nyegu,mtuhumiwa wa tatu ni John Odemba Aweyo, mtuhumiwa wa nne ni Nathan John Msuya na mtuhumiwa wa tano ni Antero Boniface Assey.

Akisoma kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba mbili ya mwaka 2022 wakili wa serikali Tumaini Kweka ameyataja mashtaka hayo kama ifuatavyo

Shtaka la kwanza ni la kuongoza genge la uhalifu, shtaka linalo wahusu washtakiwa wote ambalo wanadaiwa kulitenda mwezi  February mwaka jana  huko Wilayani Hai.

Shtaka la pili linamhusu Sabaya mnamo February 22 ,2021 huko Wilayani Hai alishawishi na kuomba rushwa ya shilingi milioni 30 kutoka kwa Gobless Swai kama kishawishi cha kuzuia taarifa za uchunguzi za ukwepaji wa kodi. 


 
Shtaka la tatu na la nne linawahusu mshtakiwa namba mbili tatu, nne, na watano ambao ni kusaidia kutendeka kwa jinai kwamba tarehe 22,02 ,2021 huko wilayani Hai, walimsasidia Sabaya kuweza kushawishi na kujipatia manufa yasiyo stahili ya shilingi milioni 30 kutoka kwa Alex Swai.

Shtaka la nne linamuhusu Sabaya ambalo ni kutumia nafasi yake kama Mkuu wa Wilaya na kunajisi nafasi yake, ambapo walimtishia Alex  Elibariki Swai kuwa amekwepa kodi na kujipatia  milioni 30 kwa manufaa yake na wenzake.

Shtaka la mwisho ni la utakatishaji  fedha ambalo linawahusu washtakiwa wote kwa pamoja ambapo  tarehe 22,02,2021 washtakiwa kwa pamoja kwa nia moja walijipatia milioni 30 huku wakijua fedha hizo ni zao la uhalifu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad