Jimbo la Ohio nchini Marekani linatazamia kutunga sheria inayowaruhusu Waalimu na Wafanyakazi wengine kubeba bunduki shuleni ambapo kabla ya kupewa mafunzo ya jinsi ya kuzitumia na kuruhusiwa, historia zao zitatazamwa zitatazamwa kwanza.
Uamuzi huu unatarajiwa kuwawezesha Walimu wenye silaha kupunguza mashambulio ya mara kwa mara ya ufyatuaji risasi yanayotokea shuleni yakisababishwa na Wanafunzi au Watu wasio Wanafunzi tabia ambayo inaonekana kuwa sugu nchini Marekani.
Mswada huo umepitishwa na mkutano mkuu wa Ohio pamoja na Chama cha Republican wiki hii huku Gavana wa Ohio Mike DeWine akisema atatia saini muswada huo huku wanaounga mkono wakisema utawaruhusu Wafanyakazi/Walimu kukabiliana na mashambulizi na kujihami kabla ya Polisi kufika eneo la tukio pale mashambulizi yanapotokea.
Hata hivyo muswada huu umepingwa na Vyama vya Walimu na Chama kikuu cha Polisi wa jimbo hilo wakisema hii itafanya litafanya shule kuwa katika hali ya hatari zaidi kwa Watoto ikiwa ni siku ya 10 zimepita toka kijana aliyekuwa na bunduki aina ya AR-15 kushambulia shule moja huko Uvalde, Texas na kuua Wanafunzi 19 na Waalimu wawili. #MillardAyoUPDATES