Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro ametembelea eneo la Changarawe, Mafinga mkoani Iringa ilipotokea ajali ya Caster jana na kuua watu 20.
Iringa. Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Simon Sirro amewatembelea majeruhi wa ajali iliyoua watu 20 na kujeruhi wengine saba katika eneo la Changalawe, Mafinga mkoani Iringa.
Ajali hiyo iliyotea jana Ijumaa baada ya basi dogo aina ya Costa kugonga lori lililokuwa limeharibika na kusababisha vifo vya watu 20.
IGP Sirro amewatembelea majeruhi ha oleo Jumamosi Juni 11, 2022 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa ambako baadhi yao walihamishiwa jana baada ya kubainika wanahitaji matibabu zaidi.
Pia, ametembelea eneo la Changarawe ambalo ajali hiyo imetokea. Eneo hilo pia ndiko ambako basi la Majinja liliangukiwa na kontena la lori mwaka 2015 na kuua zaidi ya watu 40.
Akizungumza katika ziara yake, IGP Sirro amewataka Watanzania kuwa makini kwa kutokubali kupanda magari bila kupewa tiketi ambayo ni mkataba kati ya abiria na mmiliki.
Kuhusu suala la kuruhusu magari ya abiria kufanya safari zake usiku, Sirro amesema jeshi hilo limependekeza baadhi ya njia kuanza kusafirisha abiria usiku.