MKURUGENZI wa Ufundi na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Injinia Hersi Said amesema kuna mambo mengi amepanga kuifanyia klabu hiyo endapo wanachama watampa ridhaa ya kuwa Rais wa klabu hiyo.
Akizungumza na Spotileo, kiongozi huyo amesema anataka kuifanya Yanga kuwa klabu ya mfano na yenye mafanikio kama klabu za Zamalek, Al Ahly, Waydad Casablanca na nyingine.
"Nina malengo makubwa sana na timu hii mipango yangu ni kuwa kiongozi kijana nitakayetengeneza historia itakayodumu kwa vizazi vijavyo, chini yangu Yanga itakuwa mfano wa Barcelona," amesema Hersi.
Uchaguzi mkuu wa klabu hiyo unatarajiwa kufanyika Julai 10, na mchakato uliopo sasa baada ya kuchukua na kurudisha fomu kukamilika ni Kamati husika kupitia majina ya waombaji na kupokea mapingamizi.
Kusema ukweli hapo hakuna kiongozi kama watamchagua kwa nguvu ya GSM ila Hersi hakuna kiongozi hapo
ReplyDelete