Jaji Mkuu wa Kenya Martha Koome.
Jaji Mkuu wa Kenya Martha Koome anataka mahakama ya rufaa kutangaza kwamba Rais Uhuru Kenyata amekiuka katiba ya nchi hiyo kwa kushindwa kuwateuwa majaji sita katika ya majaji 40 walioteuliwa na Tume ya huduma za mahakama (JSC) miaka mitatu iliyopita.
Bi Koome pia anataka mahakama itangaze kwamba suluhu ya madai ya kukiuka ni kuondolewa ofisini kwa Rais. Katika rufaa dhidi ya uamuazi wa Mahakama ya juu zaidi Uhuru Kenyatta aliagizwa kuwateuwa majaji sita na iwapo atashindwa kufanya hivyo Jaji mkuu achukue jukumu la kutekeleza hilo. Bi Koome amekataa hata hivyo kufanya kazi ya rais.
Badala yake, amependekeza kutangazwa kwamba Rais amekiuka kipengele cha 3(1) na cha 166(1)(b) cha katiba au maagizo.