Mchambuzi wa Michezo nchini Tanzania Jemedari Said Kazumari amekosoa maamuzi ya Uongozi wa Simba SC ya kumfuta kazi Kocha Mkuu Franco Pablo Martin, kwa kigezo cha kushindwa kufikia lengo msimu huu 2021/22.
Simba SC ilitangaza kuachana na Kocha huyo kutoka nchini Hispania jana Jumanne (Mei 31), kwa makubaliano ya kuvunja mkataba yaliyofikiwa na pande zote mbili.
Jemedari amepinga maamuzi hayo akiwa kwenye Kipindi cha Michezo cha Sports HQ cha EFM Radio, leo Jumatano (Juni Mosi).
Jemedari amesema: “Haikuwa sahihi kwa Simba SC kumtimua mkufunzi Pablo Franco Martin kwa sababu, Msimu mmoja kabla ya ujio wa Pablo, Simba SC iliwauza Chama na Miquisone ambao walikuwa na goal involvement ya magoli 40+ replacement yake ni Sakko, Banda, Kibu Dennis, Jimmyson, Kisubi Duncan Nyoni, Kanoute n.k
Edo Kumwembe: Viongozi Simba SC wanapambana kuivunja timu yao
“Wachezaji hao wote hawakuwa na mchango mkubwa msimu kulingana na Chama na Miquissone.”
“Pia hawakuwa kwenye maono ya kocha mpya ‘Pablo’ hivyo kama kuna watu walipaswa kutimuliwa Simba SC basi ni wale waliohusika kwenye usajili wa wachezaji hao.”