Justin Bieber Afunguka "Yesu Yupo Nami Ntapona Hili Tatizo Nililonalo"

 


Nyota huyo wa muziki alithibitisha wiki iliyopita kwamba anakabiliwa na tatizo la kiafya lililosababisha kupooza upande mmoja wa uso wake. Tangazo hilo lilifuatia kuahirishwa kwa matamasha yake matatu.


“Ninafahamu dhoruba hii itapita lakini wakati huo huo Yesu yuko nami ,” Bieber aliandika kwenye Instagram.


Bieber mwenye umri wa miaka 28-alisema Jumamosi kwamba hali ya kupooza kwake imetokana na maradhi yanayojulikana kama Ramsay Hunt syndrome.


Maradhi haya hutokea wakati vimelea wanaposhambulia neva za uso karibu na masikio ya mtu.


Dalili zinaweza kuwa ni pamoja na vipele vinavyosababisha maumivu katika kuta za ndani na masikio, pamoja na kuhiusi kizunguzungu.


Kama ilivyo kwa Bieber, hali hiyo inaweza kusababisha kupooza upande mmoja wa uso ambao umeshambuliwa na virusi.


Jumatatu, Bieber alituma kwenye ukurasa wake wa hadithi ya Instagram- Instagram story, akisema kuwa “alitaka kushirikisha umma sehemu ndogo ya jinsi amekuwa akihisi”.


“Kila siku imekuwa bora zaidi na katika maumivu yote haya nimepata Faraja katika yule aliyeniniumba na anayenifahamu ,” aliandika Mcanada huyo.


“Ninakumbushwa kuwa anajua mambo yangu mimi yote. Anajua mabaya yangu ambayo sitaki mtu yeyote ayajue na wakati wote ananikaribisha katika mikono yake ya upendo.


“Mtazamo huu umenipatia amani wakati wa thruba la kutisha ninalo likabili.”


Wiki ililiyopita, katika video ya dakika tatu aliyoituma kwa wafuasi wake milioni 240, Bieber alitabasamu na kukonyeza macho yake kuonyesha jinsi ambavyo upande wa kulia wa uso wake usivyoweza kutingisika kutokana na kupooza.


Mwimbaji huyo mzaliwa wa Canada alisema kuwa amekuwa akifanya ”mazoezi ya uso”ili kurejea katika hali yake ya kawaida”, lakini akasema hajui itachukua muda gani kupona.


Ramsay Hunt syndrome ni hali nadra sana ya kiafya. Kulingana Shirika la Marekani la magonjwa yasiyo ya kawaida, ni watu watano tu kwa watu 100,000 wanaokadiriwa kupatwa na hali hiyo kila mwaka.


Mara nyingi, watu hupona kikamilifu katika kipindi cha siku au wiki kadhaa, ingawa baadhi ya watu wanaweza kupata tatizo la kupoteza uwezo wao wa kusikia kabisa na kuharibika kwa macho.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad