Kaya 25 kuhama Ngorongoro kesho




MKUU wa Mkoa wa Arusha, John Mongella ametaja majina ya viongozi waliokubali kuhama katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kwenda Kijiji cha Msomera wilayani Handeni katika Mkoa wa Tanga.

Aliwataja akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha wakati akitoa tathmini ya mchakato wa awamu ya tatu ya wananchi waliokubali kuhama Ngorongoro kutoka kaya 25 zitakazohamia Msomera kesho.

Viongozi hao ni Mbunge wa zamani wa Jimbo la Ngorongoro, Kaika Ole Telele, Diwani wa Kata ya Eyasi, Augustino Lukumay, Diwani wa Viti Maalumu wa Kata ya Eyasi, Veronica Litiga na kiongozi wa kabila la Wadatoga.

Mongella alisema hatua hiyo inaleta matumaini katika mchakato huo na akasema viongozi hao kwa pamoja wamesema wapo tayari kuhama kwa hiari kwenda Kijiji cha Msomera.


 
Alisema viongozi hao wamesema wameamua kuhama Ngorongoro ili kuonesha njia kwa wananchi wengine waanze kujitafakari kuhama katika eneo hilo.

Lukumay alisema uamuzi wa serikali ni wa busara na ni muda mwafaka kwa wananchi wa Ngorongoro kuanza kumiliki nyumba, ardhi na kujishughulisha na shughuli za kiuchumi ambazo hawakuwahi kuzifanya tangu walipozaliwa.

Litiga alisema ameamua kuwa mfano kwa wananchi na kwamba kuhama Ngorongoro ni moja ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).


‘’Ninakwenda Msomera nikiwa na amani kwa vile naamini chama changu na serikali yangu haiwezi kunipeleka mahali ambako ni kubaya, naamini Msomera ni mahali bora kwa ajili ya wana -Ngorongoro walioteseka kwa muda mrefu kwa kukosa haki ya kuendesha shughuli za kiuchumi katika eneo la uhifadhi,’’ alisema

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad