Meneja wa TMDA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Anitha Mshighati, amesema wanajiandaa kufanya uchunguzi kubaini aina ya vilevi vinavyowekwa kwenye shisha baada ya kuonekana wavutaji wengi wanalewa haraka ukilinganisha na namna ambavyo kiburudisho hicho kinaelezwa kama ni aina ya sigara.
Aidha Mshighati amesema wanaanza kutoa maelekezo kwa kumbi zote za starehe na maeneo mengine ya mikusanyiko ya watu kutenga maeneo maalum ya kuvutia sigara ili kulinda afya za watu wengine.
"Siku ya kuvuta sigara duniani huadhimishwa Machi 31 duniani, ambayo kwa mwaka huu imebeba kaulimbiu isemayo 'Sigara ni hatari kwa mazingira' inatoa nafasi ya kuwaelimisha wananchi juu ya madhara yatokanayo na matumizi ya bidhaa hivyo, ambapo TMDA wamejipanga kutoa elimu kwa wananchi sambamba na kuzielekeza kumbi za starehe kutenga maeneo maalum ya kuvutia sigara pamoja na shisha," amesema Mshighati.