Kitasa Afrika Kusini chajipeleka Simba


 
BAADA ya Simba kumnyatia kwa misimu mitatu mfululizo bila mafanikio, hatimaye beki kisiki wa Burundi anayekipiga Afrika Kusini, Frederick Nsabiyumva amejipeleka Simba kiaina.

Misimu minne iliyopita, Simba ilikuwa mawindoni kuisaka saini ya beki huyo aliyekuwa Chippa United ya Afrika Kusini, ila ilishindikana kutokana na gharama za kuvunja mkataba na matakwa binafsi kuwa makubwa zaidi ya bajeti ya Simba.

Katikati ya msimu uliopita alimaliza mkataba na Chippa na kugoma kuongeza mwingine kutokana na timu hiyo kushindwa kumuongezea maslahi na kurejea Jomo Cosmos aliyoanzia maisha alivyotua Afrika Kusini kumalizia msimu na sasa yupo huru.

Mwanaspoti lilipiga stori na beki huyo juzi baada ya mechi ya timu ya taifa ya Burundi iliyofungwa mabao 2-1 na Cameroon kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa na kusema kwa sasa yupo tayari kujiunga na Simba.

“Misimu iliyopita kulikuwa na mazungumzo na Simba, ila hayakutimia kwa kuwa nilikuwa na mkataba na Chippa. Sasa niko huru na nipo tayari kuzungumza na timu yeyote,” alisema.

“Simba ni timu bora na inashiriki mara kwa mara michuano ya kimataifa hivyo hakuna mchezaji atagoma kuichezea kama wataelewana, ndio maana nimesema kama watahitaji huduma yangu basi ni suala la maongezi tu na tukifikia makubaliano basi nitasaini.” Simba inatafuta beki wa kati mwenye ubora kusaidiana na Henock Inonga na Joash Onyango msimu ujao wakishaachana na Pascal Wawa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad