Pompeii: Kobe wa zamani mjamzito awashangaza wanaakiolojia
Wataalamu wanaamini kuwa kobe huyo alikuwa akitafuta mahali pazuri pa kutagia yai lake wakati maafa ya volkano yalipotokea mwaka wa 79 AD.
Mlima Vesuvius ulipolipuka karibu miaka 2,000 iliyopita wakaaji wa kale wa Pompeii waligandishwa papo hapo na kuwa majivu.
Vivyo hivyo pia iliibuka kuwa mimea na wanyama wa jiji hilo - pamoja na kobe mjamzito na yai lake.
Wanaakiolojia waligundua mabaki ya kobe huyo yakiwa yamezikwa chini ya majivu na mwamba ambapo alikuwa ametaga mayai ambayo hayakuwa yamegunduliwa tangu mwaka wa 79 AD.
Kobe huyo alikuwa amejificha chini ya jengo ambalo tayari lilikuwa limeharibiwa wakati maafa ya volkano yalipotokea.
Wanaakiolojia walipata mabaki hayo walipokuwa wakichimba eneo la jiji ambalo wakazi wake wa kale walikuwa wakijenga upya baada ya tetemeko la ardhi la awali kuharibu Pompeii mwaka 62 AD.
Takriban miaka 2,000 iliyopita kobe wa 14cm (inchi 5.5) alikuwa amejichimbia kwenye shimo dogo la chini ya ardhi chini ya duka lililoharibiwa katika tetemeko hilo la awali.
Wataalamu wanasema ukweli kwamba alipatikana na yai unaonyesha kwamba aliuawa wakati akijaribu kutafuta mahali penye utulivu ili kuweka watoto wake.
Nyayo za binadamu wa kale zaidi zapatikana na kufichua mengi3 Oktoba 2021
Fahamu 'maisha ya siri' ya watoto wa watu wa kale22 Julai 2021
Wanasayansi wagundua maiti ya kale ya mwanamke mjamzito30 Aprili 2021
Kobe huyo mjamzito aligunduliwa kando na yai lake
Maelezo ya picha,
Kobe huyo mjamzito aligunduliwa kando na yai lake
Mwanaakiolojia wa Chuo Kikuu cha Oxford, Mark Robinson, ambaye aligundua mabaki ya kobe mwingine katika eneo la karibu na Pompeii mwaka wa 2002, aliiambia BBC kulikuwa na maelezo mawili ya jinsi kobe huyo alifika hapo.
‘’Moja ni kwamba ni kobe kipenzi ambaye labda alitoroka na kwenda kwenye yale yalikuwa magofu ya tetemeko kubwa la ardhi.’’
Uwezekano mkubwa zaidi ni kwamba alikuwa kobe kutoka Kijiji jirani ambaye alikuwa ametangatanga katika jiji la kale, alisema.
‘’Pompeii iliharibiwa kwa kiasi kikubwa na si kila mahali pangeweza kujengwa upya baada ya tetemeko hilo. Mimea na wanyama kutoka maeneo ya mashambani ilikuwa imehamia mjini.’’
Kobe huyo aligunduliwa katika uwanja mdogo chini ya sakafu ya kale ya jengo la Pompeii. Wataalamu wanasema ugunduzi huo unaonyesha utajiri wa mfumo wa ikolojia wa Pompeii katika kipindi baada ya tetemeko la ardhi.
‘’Jiji lote lilikuwa eneo la ujenzi, na ni dhahiri baadhi ya maeneo hayakutumika hivi kwamba wanyama pori waliweza kuzurura, kuingia na kujaribu kutaga mayai yao,’’ mkurugenzi mkuu wa Pompeii, Gabriel Zuchtriegel alisema.
Mgeni mmoja wa Pompeii, mwanafunzi wa Finland ambaye alikuwa akipita karibu na eneo hilo wakati ugunduzi huo ulipofanywa, alielezea kile alichokiona kwa BBC kuwa ‘’cha kuvutia.’’
‘’Walikuwa wameondoa ganda la mnyama, kwa hivyo kilichoonekana ni mifupa na yai,’’ Joonas Vanhala alisema.
‘’Ilikuwa ya hudhurungi, rangi ya mchanga.’’
‘’Nisingetambua kuwa ni yai kama wasingeniambia,’’ aliongeza
Yai halikuweza kudumu