Kufuatia Sakata la Mtoto wa Miaka 8 Kuuawa, Wazazi Waibua Mazito "CCTV Camera Zilikuwa Zimezimwa"


SAKATA la mtoto mwenye umri wa miaka 8 anayedaiwa kunyongwa na msichana wa kazi eneo la Kimara Temboni mtaa wa Sokoine jijini Dar es salaam limechukua sura mpya baada ya mzazi kuthibitisha kuwa CCTV Camera zilikuwa zimezimwa.

Baada ya Global TV kwenda nyumbani kwa Marehemu imefanya mahojiano na wazazi wote wa marehemu ambao wote kwa pamoja wamethibitisha kuwa na sintofahamu kutokana na utata wa mazingira ya kifo cha mtoto wao anayefahamika kwa jina la Erickson.


Erick Kimaro Baba wa marehemu akihojiwa na mwandishi wa Global TV Imelda Mtema
Mama wa marehemu anadai alikuta alama za michubuko katika shingo ya marehemu pamoja na uvimbe juu kidogo ya jicho lakini Baba wa marehemu anayefahamika kwa jina la Erick kimaro Mumba naye alipofanya mahojiano alisema wasiwasi ulikuwa pale walipouona mwili wa marehemu ukiwa na michubuko maeneo ya shingoni mwake ndipo wakahisi pengine anaweza kuwa amenyongwa.

Madai ya kwamba CCTV Camera ilinasa tukio zima ni madai yaliyokanushwa na Baba wa Marehemu akidai kuwa CCTV Camera ilikuwa imezimwa muda wote tangu siku moja kabla ya tukio hilo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad