Kwa huzuni mwanadada Kelly(41) kutoka nchini Uingereza amesema kila siku inamlazimu kuoga sio chini ya mara nne kwasababu amezaliwa na tatizo la kutoa harufu mbaya kama samaki aliyeoza na hali hiyo hujionesha hadi katika mkojo
Kelly amesema alianza kujigundua kuwa ana harufu ya tofauti akiwa na miaka 6 tu lakini hakujua hasa tatizo hilo linatokana na nini hadi alipofikisha miaka 34 ndio akaelewa vizuri
Amesema inamlazimu kuoga mara nne kwa siku na kujipulizia pafyumu/deodorant kila wakati lakini ndani ya muda mfupi tu tatizo linarudi tena. Amesema ametumia sabuni za kila aina kuogea lakini wapi sana sana mwili ukiwa katika uasili wake kidogo kuna afadhali
Ameongeza kuwa baadhi ya watu wasiojua tatizo hilo humsema vibaya wakidhani sio msafi mara unene ndio chanzo apungue lakini anasema ukweli ni tofauti kwani alipokuwa mwembamba hali ilikuwa hivyo hivyo na pia yeye ameajiriwa sekta ya afya(radiographer) hivyo watu kudhani labda ni mchafu inamfanya ajisikie vibaya hadi kulazimika kwenda kwa wanasaikolojia na hata kazini anapendelea zaidi zamu za usiku
Amesema akikaa karibu na watu anaonekana kama kero flani hivi. Pia kuna baadhi ya vyakula kama maini, figo, maharage, karanga etc hatakiwi kula kwani vinachochea ukubwa wa tatizo hilo na Kuna vyakula ameshauriwa ale kupunguza ukali wa tatizo
Katika lugha rahisi tatizo hilo linajulikana kama Fish-Odour Syndrome na hadi sasa rekodi za dunia zinaonesha watu 100 tu ndio wana tatizo hilo lakini wataalam wanasema kuna uwezekano wapo watu wengine kukaribia hata 200 ambao rekodi zao bado kukusanya
Watu wenye tatizo hilo wengine hutoa harufu Kama ya samaki waliooza, kinyesi etc. Na inaelezwa wataalam bado hawajagundua dawa ya kuondoa au kuponesha tatizo hilo moja kwa moja
Kelly amesema ameamua kuzungumza kuhusu hali yake ilimkutoa elimu kwa wasiofahamu hali hiyo