Lipumba Akosoa Vitambulisho vya Taifa Kuunganishwa na Ulipaji Kodi

 


Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amesema Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Mchemba  amefanya makosa  ya kimkakati kuunganisha vitambulisho vya Taifa na ulipaji wa kodi huku akieleza  Itaathiri motisha ya wananchi kujisajili kupata vitambulisho hivyo.


Juni 14,2022  wakai waziri huyo akiwasilisha bajeti ya mwaka 2022/23, alisema Serikali inakusudia kutoa namba ya utambulisho wa mlipakodi (TIN) kwa kila Mtanzania mwenye umri wa kuanzia miaka 18 au zaidi kwa utaratibu wa usajili wa namba ya utambulisho wa Taifa.


Amesema hadi sasa Serikali haijakamilisha shughuli ya kuwapatia vitambulisho vya Taifa Watanzania wote baada ya zaidi ya miaka kumi toka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) kuanzishwa hivyo ni muhimu Serikali ikajikita kuharakisha wananchi kupata vitambulisho vyao.


"Vitambulisho vya kitaifa na teknolojia ya kielektroniki ni nyenzo ya kuongeza kasi ya maendeleo. Ni makosa makubwa ya kimkakati hivi sasa kuunganisha vitambulisho vya taifa na ulipaji wa kodi."


"Itaathiri motisha ya wananchi kujisajili kupata vitambulisho vya kitaifa. Waziri wa fedha anarejesha kinyemela kodi ya kichwa kupitia vitambulisho vya Taifa. Hili halikubaliki. Utozaji wa kodi uambatane na uwezo wa kuilipa."


"Kasi ya watu kujiandikisha kupata vitambulisho itapungua kwani kila mtu ataamini akipata namba ya kitambulisho atakuwa analipa kodi," amesema

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad