Madaktari wannne, wauguzi na mwanasaikolojia, aliyekuwa akimuhudumia nguli wa mpira wa miguu duniani, Diego Maradona, watashitakiwa kwa kosa la mauaji.
Maradona alikuwa akisumbuliwa na tatizo la Hematoma, alifanyiwa upasuaji wiki chache kabla ya kifo chake kilichotokana na mshtuko wa moyo.
Waendesha mashitaka wanaamini kifo cha Maradona, kilitokana na uzembe wa madaktari, wauguzi na mwanasaikolojia, wakidai watu hao hawakufanya kazi yao kwa umakini hivyo kusababisha kifo chake.
Shtaka hilo linaweza kuwa na adhabu ya kifungo cha miaka minane hadi 25 jela, endapo watakutwa na hatia ya kufanya uzembe uliogharimu maisha ya mwanasoka huyo wa wazamani kutoka taifa la Argentina.