Malota Soma Aitetea Simba "Uchovu Umeigharimu Simba SC Kukosa Kombe"

 

Mshambuliaji wa zamani wa Simba SC Malota Soma ‘Ball Juggler’ amesema kama isingekua kuchoka kwa wache
zaji wa Simba SC baada ya kufanya kazi nzuri kwa misimu minne mfululizo, klabu hiyo ingefanikiwa kutetea taji la Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara ya tano mfululizo msimu huu 2021/22.


Malota Soma ambaye alitamba na Klabu za Reli Kilosa na Reli Morogoro kabla ya kutua Simba SC, ametoa kauli hiyo baada ya kuiona Young Africans ikitawazwa kuwa Mabingwa wa Tanzania Bara kwa mara ya Kwanza baada ya Miaka minne.


Amesema Simba SC ilikua na nafasi kubwa ya kuendeleza ufalme wa Soka la Tanzania Bara, lakini bahati mbaya asilimia kubwa ya wachezaji wake wamechoka, kwa kazi walioifanya katika Ligi ya ndani na Kimataifa.


“Binafsi ninawapongeza wachezaji wa Simba SC licha ya kushindwa kufanya vizuri msimu huu, wameonesha uwezo wa kupambana na kuwa nafasi ya pili, wamecheza kwa kujituma na hawajavunjika moyo licha ya kupoteza ubingwa,”


“Mchezaji kucheza kwa miaka minne mfululizo na kupata mafanikio katika Ligi ya ndani na kutikisa Afrika sio jambo dogo, uchovu umewafelisha Simba SC msimu huu, lakini bado ninasisitiza pongezi kwa wachezaji, wameonesha ubora wao na kuifikisha timu ilipo sasa.” Amesema Malota Soma


Simba SC imeshajihakikishia kumaliza nafasi ya pili ikiwa na alama 57 ambazo haziwezi kufikia na klabu yoyote katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, huku ikisaliwa na michezo mitatu mkononi, baada ya kucheza na KMC FC jana Jumapili (Juni 19) na kuibuka na ushindi wa 3-1.


Young Africans ipo kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na alama 67, ambazo zinaitofautisha na Simba SC kwa alama 10.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad