Maneo na Chokochoka za Baadhi ya Viongozi wa SIMBA zamfikia Barbara Asema Haya "Nijiuzulu Kwa Lipi Labda"




YALE makombora na kelele nyingi dhidi yake ikiwamo kuelezwa eti amejiuzulu, zimemfikia Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez na kuamua kuvunja ukimya

Barbara amekuwa akitetwa na baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, kuwa amekuwa haambiliki kwenye maamuzi kadhaa hususani yanayohusu fedha. Katika mahojiano maalumu na Mwanaspoti, Barbara alisema kila kitu amekuwa akikisikia na kukiona kwenye mitandao ya kijamii.

“Kama kuandika barua na kuacha kazi hii ningefanya mwaka jana nikiwa mgeni katika soka, ila nilipiga moyo konde nilipambana na nikavuka wakati huo hadi kufika hapa,” alisema Barbara na kuongeza hana mpango wa kuandika barua ya kujiuzulu kisa kutetwa na watu wachache kwenye Bodi ya Wakurugenzi au nje ya hapo. “Jambo hilo la kutokuwa na maelewano sio la kweli, kwani nimekuwa nikifanya nao kazi kwa maelewano makubwa na kupokea maelekezo kutoka kwao, sasa sijui haya mengine yanatokea wapi?” alisema Barbara

“Shughuli zote za klabu kila siku zinakwenda chini yangu na nimekuwa nikifanya kila ambacho naagizwa kutoka kwa Mwenyekiti na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, kwani wao ndio mabosi zangu, lazima nifanye kazi vile wao wanahitaji.”


“Pia wapo wengine wamekuwa wakinishambulia na kusema mambo mengi, hawapo uongozini kwa sasa, lakini kwangu naona ni changamoto ya kuzidi kupambana kuhakikisha nafanya kazi kwa ufanisi zaidi ili kuhakikisha tunaifikisha Simba kwenye malengo iliyojiwekea,” alisema Barbara na kuongeza;

“Haya yote yanatokea kwa sababu Simba tumeshindwa kufikia malengo yetu ya kufika nusu fainali Kombe la Shirikisho Afrika, kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho (ASFC). Kama tungefanya vizuri na kufikia malengo ikiwemo kubeba mataji, haya yote yasingetokea.”

Mtendaji huyo alisema hata hivyo yeye hana kinyongo kwa vile anachukua hayo yote kama changamoto kwenye kazi.


“Haiwezi tokea hata siku moja kutoa mbele na kuanza kujibu mambo mengine nayaacha yapite tu kama ilivyokuwa kama mengine ya huko nyuma akili na nguvu yangu nimeiweka kwenye mambo muhimu ya klabu,” alisema.

“Siwezi kukatishwa tamaa au kuondoka kwenye malengo muhimu ya timu kuona jinsi gani msimu huu maeneo yapi yalitifanya tushindwe kuwa bora na kushindwa kufikia malengo ili kuboresha na kuwa kikosi imara msimu ujao kuchukua tena mataji.

“Mashabiki wa Simba wasiwe na wasiwasi viongozi tunafahamu changamoto msimu huu zilikuwa wapi tupo kwenye vikao muhimu vya ndani kuisuka tena timu upya katika maeneo muhimu na naimani tutarudi kwenye kiwango bora bila ya kujali mitihani tunayokutana nayo wakati huu.”

Baadhi ya wanachama wakongwe wa Simba wamesikika kwenye redio mbalimbali za Dar es Salaam wakimtuhumu bosi huyo kwa kufanya maamuzi mengi bila kuwapa nafasi tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma ambapo usajili ulifanywa na kamati na makundi maalum.


Simba iliondolewa Ligi ya Mabingwa Afrika mapema na kuangukia Kombe la Shirikisho Afrika na kukwamia robo fainali, huku ikipoteza mechi ya nusu fainali ya ASFC na kupoteza taji, ilihali katika Ligi Kuu Bara kuna dalili za kulitema pia kombe.

Kukwama kwenye malengo hayo yameufanya uongozi kuachana na Kocha Pablo Franco
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad