“Oscar Oscar sio tu mfanyakazi mwenzangu, ni rafiki ambaye pia tumeshirikiana kwenye biashara na hata mambo binafsi. Tanzania inakumbuka kuwa alipotaka Urais wa TFF, niliamua kumpeleka kuchukua fomu nikiwa kama dereva wake. Wiki chache zilizopita nilipata msiba na Oscar alinipeleka kijijini tukakaa kama wiki lakini hakuaniambia kuwa anaondoka kwenye Sports HQ.
.
Nimesikitika, nimeumia, kama rafiki na kama shabiki wa Sports HQ, kumkosa Oscar ni jambo gumu.
.
Umekuwa wakati mbaya sana kwangu kwa sababu wakati nawaza pengo la Oscar, dada yetu Dina Marios naye kwa sababu anazozijua, au pengine alishauriana na Oscar, hatutakuwa naye kwenye Uhondo.
Dina ni nguli aliyeamua kuwa EFM kuanzia chini, akakubali kuja kwa redio iliyoitwa ya mchangani, akasaidiana nasi kukua na yeye akikua zaidi. Niseme kweli, pengo lake litakuwa kubwa mno.
.
Hata hivyo hii ni kazi, nawatakia kila la heri kwenye majukumu yao mapya.
Sisi kama Taasisi, tunahitaji muda kutoa tamko rasmi na kueleza yanayofuata baada ya hili. Panapo majaaliwa kesho jioni tutaongea rasmi.
.
Kila la heri Ndugu zangu Oscar na Dina.” @majizzo