Matola ''Tunataka Kumaliza ligi kwa Heshima''

 


Kaimu Kocha Mkuu Seleman Matola, ameweka wazi kuwa lengo lao lililobaki ni kuhakikisha wanamaliza ligi kwa heshima baada ya kuwa na nafasi ndogo ya kutetea ubingwa msimu huu.


Matola amesema wanahitaji kushinda mechi zote tano zilizobaki kwa ajili ya kuweka heshima na kuwapa furaha mashabiki.


''Maandalizi kuelekea mchezo wa dhidi ya Mbeya City yanaendelea vizuri baada ya wachezaji waliokuwa kwenye majukumu ya timu ya taifa wamerejea na wamefanya mazoezi na wenzao'' amesema Matola


Aidha Matola ameongeza kuwa wachezaji Medie Kagere na Peter Banda ndiyo pekee ambao hawajarudi lakini wanataraji kutua nchini muda wowote kuanzia sasa.


“Hatuna nafasi ya kutetea ubingwa lakini tunataka kuweka heshima kwa kushinda mechi zote tano zilizobaki ili kuwapa furaha mashabiki wetu,” amesema Matola.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad