Mil 700 kwa atakayempata Mchina aliyemuua mwenzake



 
Familia ya Fu Nannan (Pichani) ambaye ni raia wa China aliyeuawa Juni 11, 2022, kwa kupigwa risasi nyumbani kwake Ilala Jijini Dar es Salaam na Mchina mwenzie aitwaye Zheng Lingyao, imeahidi dau la shilingi milioni 700 kwa atakayefanikisha kupatikana kwa mtuhiwa huyo.
Fu Nannan, aliuawa kwa risasi wakati akiamua ugomvi kati ya mwanamke aitwaye Nie Mnqin, ambaye inadaiwa aliwahi kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na mtuhumiwa, na mwili wake umezikwa leo Juni 26, 2022, Mikocheni Dar es Salaam.

Wakizungumza na EATV katika mazishi ya Fu mapema leo Mikocheni Dar es Salaam, wafanyakazi na wakazi wa Kitongoji cha Madodo, Mkuranga kilipo kiwanda cha marehemu wamesema mbali na fursa za ajira walizozipata marehemu amekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya jamii hiyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad