Mke wa aliyenusurika kuuawa na washirika wa Burna Boy afunguka

 


Mwanamke mmoja aliyetambulika kwa jina la Briella Neme, ameitumia akaunti yake ya Instagram (Insta Story), kuweka wazi sintofahamu iliyoibuliwa na ghasia za kutisha zilizobabishwa na mwanamuziki wa Nigera Burna boy katika klabu ya usiku.


Kwa mujibu wa mrembo, huyo amesema kuwa usiku huo ulikuwa ni wa kuvinjari baina yake na zaidi ya watu ishirini wa familia yake akiwamo mume wake, wakiwa katika ukumbi wa starehe mpaka muda ambao kisa hicho chenye kumuhusisha Burna Boy kilipotokea.


Katika simulizi yake kwenye Insta stori, Briella amesema alizingirwa na kushikwa kwa zaidi ya mara tatu na wanaume walioagizwa na Burna Boy, wakimuomba akutane naye jambo ambalo mrembo huyo hakukubaliana nalo.


“Katika jaribio la kwanza niliwaambia sihitaji kuonana wala kuongea na Burna Boy na nimeolewa nina mwenzangu, wakaja tena mara ya pili nikawajibu hivyo hivyo, wakaja mara ya tatu na hivyo kusababisha marafiki zetu kuchukizwa huku wakihoji kwa nguvu kwa nini aliendelea kunisumbua licha ya kukataa,” alisimulia.


Briella ameweka wazi kuwa baada ya rafiki zake na watu wa karibu kuchukizwa na kitendo hicho kulitokea fujo kubwa klabuni hapo, ambapo mumewe pamoja na rafiki yake mmoja walishambuliwa kwa risasi katika sehemu kadhaa katika miili yao.


Mrembo huyo amebainisha kuwa ilimchukua takribani siku nne mmiliki wa klabu hiyo ya usiku, Obi Cubana kuwafikia baada ya tukio hilo la kutisha ili kushughulikia upatikanaji wa maelewano baina yake na wateja wake.


Habari za Burna Boy na washirika wake kuibua ghasia kiasi cha kuhatarisha maisha ya watu waliohudhuria kwenye furaha kwenye klabu hiyo ziliibuka wiki kadhaa zilizopita.


Ambapo watu kadhaa walioshuhudia tukio hilo walitoa maelezo ya jinsi mwimbaji huyo na wafanyakazi wake walivyofanya mambo yasiyo ya kiustaarabu na kusababisha madhara kwa watu na mali katika klabu hiyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad