Mombasa: Makahaba Waongeza Bei Kutokana na Hali Ngumu ya Kiuchumi




Makahaba hao walisema kuwa kupanda kwa bei za bidhaa za msingi nchini kumewafanya kuongeza bei kwa huduma zinazotolewa
Bei hizo mpya zitaanza kutekelezwa Alhamisi, Juni 30 na tayari wamewapa wateja wao notisi ya siku 3 siku ya Jumatatu
Kupitia shirika la kutetea haki yao, wameombwa kuzingatia kwa dhati bei mpya zilizowekwa, na iwapo watakiuka watachukuliwa hatua za kinidhamu
Wafanyabiashara ya ngono kutoka kaunti ya Mombasa wametoa wito kwa wateja wao kuchimba zaidi mifukoni mwao ili kufurahia huduma zao kutokana na hali mbaya ya kiuchumi inayoshuhudiwa nchini.

Mombasa: Makahaba Waongeza Bei Kutokana na Hali Ngumu ya Kiuchumi.
Mombasa: Makahaba Waongeza Bei Kutokana na Hali Ngumu ya Kiuchumi. Picha: UGC.
Shirika la kutetea haki za wafanyabiashara ya ngono Nkoko Injuu Africa (NGO), kupitia kwa mratibu wake Lucy Kiragu, ilisema kuwa kupanda kwa bei za bidhaa za msingi nchini kumewafanya kuongeza bei kwa huduma zinazotolewa.

Nkoko Injuu lina zaidi ya wanachama 4000 waliosajiliwa kote kaunti ya Mombasa.

"Tumekubaliana juu ya bei ya msingi ya kutoza, kwa kikao kisicho na mapenzi sasa kitauzwa Ksh500 kutoka Ksh300, kwa vifurushi kamili pamoja na mapenzi gharama zetu sasa ni Ksh 1000 kutoka kwa bei ya kawaida ya Ksh500, hii ni wakati mtu anatumia ulinzi. . Wale wanaotaka kufurahia huduma bila ulinzi watahitajika kutoa Ksh3000," Kiragu alisema.


 
Ana Mengi: Gavana Kingi Azungumzia Kilichomfanya Kutohudhuria Mkutano wa DP Ruto
Kiragu alisema bei hizo mpya zitaanza kutekelezwa Alhamisi, Juni 30 na tayari wamewapa wateja wao notisi ya siku 3 siku ya Jumatatu.

Pia alitoa wito kwa wanachama wao kuzingatia kwa dhati bei mpya zilizowekwa, na iwapo watakiuka watachukuliwa hatua za kinidhamu.

"Wakati mgumu unahitaji hatua kali. Ikiwa mtu hayuko tayari kuzingatia sheria zilizowekwa, atakabiliwa na faini kubwa na hata kufutiwa usajili na shirika. Tunatoa wito kwa wanachama wetu kutoa ushirikiano na kuanzisha na kushikamana na bei mpya," alisema.


Kiragu aliongeza kuwa idadi ya wateja walio tayari kufurahia huduma zao imepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na hali ngumu ya kiuchumi iliyopo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad