Pitso Mosimane moja ya makocha wakubwa barani Afrika
KOCHA wa Klabu ya Al Ahly raia wa Afrika Kusini Pitso Mosimane ameachana rasmi na mabingwa wa Misri kwa maubaliano ya pande zote mbili.
Klabu ya Al Ahly imetoa taarifa kupitia ukurasa wake rasmi wa Twitter ikiandika:
“Al Ahly na Pitso tumefikia makubaliano ya kutengana.”
Kulikuwa na taarifa hivi karibuni za Mosimane kutokuwa na uhusiano mzuri na Klabu ya Al Ahly ambapo ilimlazimu Meneja wao Moira Tlhagale kupanda ndege na kwenda Cairo kwa ajili ya maongezi na uongozi wa Al Ahly.
Mosimane amefanikiwa kuchukua makombe 5 akiwa na Al Ahly
Taarifa za ndani zinabainisha uwa Mosimane ndiye aliyepelea barua ya kuomba kujiuzulu kama kocha wa Klabu hiyo, barua ambayo ilijadiliwa na uongozi wa Al Ahly chini ya Rais wa Klabu hiyo Mahmoud El Khatib pamoja na Mwenyekiti wa klabu hiyo Hossam Ghaly ambao pia walishirikisha Bodi ya Wakurugenzi waliopitisha maamuzi hayo ya Mosimane.
Taarifa za kuthibitika ni kwamba Mosimane atandoka pamoja na baadhi wa watendaji wake kwenye benchi la ufundi akiwemo Kabelo Rangoaga, Musi Matlaba pamoja na Kyle Solomon.
Mosimane amefanikiwa kushinda makombe matano akiwa na Mabingwa hao wa muda wote wa Afrika ikiwemo makombe mawili ya Klabu Bingwa Afrika aliyoshinda mfululizo tangu ajiunge na miamba hiyo mwezi Septemba mwaka 2020.