Mahakama ya Virginia nchini Marekani imetoa hukumu ikimuunga mkono mwigizaji Johnny Depp katika kesi ya kashfa dhidi ya mke wake wa zamani, Amber Heard, na kubaini kuwa alimkashifu kwa tuhuma za unyanyasaji wa nyumbani.
Depp alipewa fidia ya Sh bilioni 34.9 (dola milioni 15), ingawa hiyo inaweza kupunguzwa na sheria. Shauri la Heard lilitupiliwa mbali kwa kiasi kikubwa, huku mahakama ikikubali kuwa Depp alimkashifu katika tukio moja tu, na kutoa fidia ya dola milioni 2.
Depp alimshtaki Heard akidai fidia ya dola milioni 50, akimtuhumu kwa kashfa katika maoni ya Washington Post ya 2018 akisisitiza kwamba alikuwa akimnyanyasa nyumbani. Heard alishtakiwa kwa dola milioni 100, akisema wakili wa Depp alimkashifu kwa kuyaita mashtaka hayo kuwa ya uwongo.
Kesi hiyo ilifunguliwa Aprili 11 na kwenda kwa jopo la majaji Ijumaa iliyopita. Ilichukua siku tatu za kazi kwa mahakama ya kiraia ya watu saba huko Fairfax, Virginia kurudisha uamuzi huo kwa kauli moja.