Ili kuendelea kuimarisha demokrasia ndani ya Chama cha mapinduzi (CCM) ,Uongozi wa Chama hicho mkoa wa Njombe mara baada ya kukamilisha uchaguzi wa ndani katika ngazi ya matawi na kata umetoa wito kwa wanachama kujitokeza na kugombea nafasi za uongozi katika jumuiya za Chama hicho katika ngazi ya wilaya na mkoa.
Katibu wa siasa na uenezi wa CCM mkoa wa Njombe Erasto Ngole kwa niaba ya katibu wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Njombe ametoa wito huo mbele ya waandishi wa habari huku kigezo mojawapo katika sifa za uongozi ikiwa ni kujua kusoma na kuandika na kubainisha kuwa kuanzia Julai 2 mwaka huu nafasi za uongozi zitakuwa wazi.
Aidha Ngole amesema Chama hicho kimejipanga vyema kudhibiti changamoto mbali mbali ikiwemo matumizi ya rushwa pindi itakapojitokeza na hakiko tayari kuruhusu hayo.
“Tulianza uchaguzi ngazi ya shine tukaja Malawi na kata lakini tarihe mbili ya mwezi wa saba maka tarehe kumi kutakuwa na zoezi la uchukuaji wa fomu kenye ngazi zote kwa maana ya jumuiya na Chama ndani ya wilaya na mkoa,nafasi za uongozi zinazoombwa kwenye ngazi ya mkoa ni nafasi ya mwenyekiti,mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM taifa,katibu wa siasa na uenezi,wajumbe wawili kila wilaya watakaoingia kwenye halmashauri kuu ya CCM mkoa”alisema Erasto Ngole
Khamis Ally Kachinga ni katibu wa jumuiya ya vijana CCM mkoa wa Njombe amewataka vijana kutumia fursa hiyo katika kuomba kugombea nafasi mbalimbali ili walisaidie taifa katika kujiletea maendeleo huku katibu wa jumuiya ya wazazi Mkoa Bi.Agatha Lubuva akikemea vitendo vya rushwa wakati wa uchaguzi huo.
Vijana ndio wanatajwa kutakiwa kujitokeza kwa wingi kugombea katika nafasi mbalimbali za uongozi ambapo baadhi yao akiwemo Johnson Mgimba wanasema hawatokuwa nyuma katika mchakato huo.
Noel Mseo ni naibu mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU Mkoa wa Njombe ambaye anasema tayari wameanza kuchukua hatua mbalimbali za kufuatilia mchakato huo pamoja na kutoa elimu kwa wanasiasa wenyewe.
Uchaguzi huo unakuja baada ya viongozi wake kuhudumu katika kipindi cha miaka mitano baada ya kuchaguliwa mwaka 2017.