Ni ‘Mama Amina’ au ni Chuki Dhidi ya WCB??

 


Nimeona gumzo mtandaoni kuhusu kauli ya Mbunge Babu Tale kutolea mfano wimbo ‘Mama Amina’ wa Marioo Bungeni akitaka kuonyesha ni jinsi gani BASATA wasivyokuwa makini kwenye kusimiamia kazi za wasanii hasahasa kwenye kipengele cha matusi na kufungia nyimbo za wasanii kwa kigezo cha maadili.

Watu wengi wanakosoa kwamba kwanini ametolewa mfano wimbo wa Marioo, huku wengi wakienda mbali zaidi kwa kudai anamchongea.Hivi ni nani asiyejua kwamba wimbo ‘Mama Amina’ kiitikio chake ni matusi?.

Umewahi kuhudhuria show yoyote ya Marioo ukasikia huo wimbo unaitikiwaje? Basi tusiende mbali hata muulize mtoto wako hapo ulipo kuhusu kiitikio cha huo wimbo utamuelewa Babu Tale.

Babu Tale na hoja iliyoitwa yakifinafsi.

Babu Tale akiwa Bungeni alijikita katika maeneo matatu, moja kumshukuru Rais Samia, ndipo akaanza na BASATA na kumaliza na COSOTA vyombo ambavyo ni kwaajili ya wasanii wote.

Kwa ujumla wa hoja yake wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Sanaa iliyowasilishwa na Waziri Mchengerwa, kiujumla alionyesha kukerwa na utendaji kazi wa BASATA na COSOTA na hii ni kutokana na uzoefu wake kwenye muziki kwa miaka 20.

Kufungiwa nyimbo na BASATA

Wasanii wa WCB ni moja kati ya wahanga wakubwa wa adhabu hii kutokana na ukubwa wao na mara nyingi wamekuwa wakijitokeza hadharani kulalamika kutokana na uwekezaji mkubwa wanaoufanya kwenye project zao na huwenda kuliko wasanii wengine wa Tanzania.

Tale ambaye ni meneja wa WCB aliongea kwa uchungu kwa sababu ni jambo ambalo linamgusa moja kwa moja tena wasanii wake wanaangaliwa kwa ukaribu.

Sio kweli WCB ni tatizo.

Kuna namna tubadili namna yakufikiria, sio kila hoja au msimamo wa wasanii WCB na viongozi wao ni ubinafsi, kuna namna tunatakiwa kuchambua hoja zao na kuvaa viatu vyao kama wawekezaji wakubwa kwenye muziki.

Diamond kujitoa kwenye tuzo kwa sababu zake gumzo, wakasewa ubinafsi, Kumdai pesa msanii wake anayetaka kuachana na lebo yake, roho mbaya. Kila anayelitaja jina la Diamond au WCB kwa mazuri basi analipwa.

Kuendelea kuwa na chuki na WCB kila lao baya, kuna mengi tunayakosa, Tasnia yetu bado inawahitaji sana

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad