Nimegundua mapenzi hayanitaki, ngoja nifanye mambo mengine tu

 


Nina miaka 34 sasa nikiwa mama wa watoto 3, hakika sina budi kukubali kuwa mapenzi hayanitaki tena hayanipendi kabisaa, japo niliyapenda na kuyapa thamani katika maisha ila nimeangua sina budi kuyaacha rasmi kuanzia leo.

Historia yangu kwa ufupi,

Mpenzi wa kwanza.

Huyu alinionesha mapenzi ambayo hakika sijawahi kupata, alikuwa mkweli mpole, na mwenye mapenzi ya dhati kwangu, nami nilimpenda sana sana katikati ya penzi zito tukapata mtoto 1 kwa bahati mbaya mpenzi wangu Mungu akampenda zaidi akafariki dunia nikabaki na mtoto.

Ndiyo penzi pekee ambalo sina historia mbaya nalo, penzi hili lilidumu kwa miaka 5 na lilikuwa bado tamu ila ndo ivyo ilibidi nikubali kuwa hayupo na nisonge mbele.

Kimbembe kinaanza.

Mpenzi wa pili

Tulikutana katika mazingira ya kutafuta maisha tukaanza kuwa marafiki baadaye tukawa wapenzi, mapenzi yakaendelea japo tulikuwa na migogoro ya hapa na pale ila tunaongea tunasawazisha maisha yanaendelea.

Kushtuka nina ujauzito, nikamwambia nina ujauzito akasema sasa itakuwa aibu kubwa sana (kipindi hiko yeye alikuwa anasali kanisa fulani na mimi akanikaribisha tusali wote na alikuwa ni mtumishi kanisani hapo) akasema suluhisho ni kufunga ndoa ya haraka.

Tukaongea na wazazi, ndoa ya haraka ikapangwa, akaambiwa atoe Mahari 1,000,000 mimi nikapambana kuwaambia hii ndoa ni ya haraka hasa kuzingatia hali yangu tukichelewa tumbo litakuwa kubwa hivyo kwa sasa uwezo wake labda atoe 200000 tu, na harusi yenyewe ni ya bila sherehe.

Wazazi wakakubali, akaambiwa atoe laki mbili kumbe hana yeye akasema laki basi ikabidi wazazi wapokee tu maana ndoa ishaanza kutangazwa, harusi ikafungwa bila sherehe.

Baada ya ndoa, ilikuwa ni migogoro kama tunaigiza sinema ndani, yaani ni ugomvi kila kikucha kila siku tunasuluhisha kesi, tukipatana na siku 3 zilizobaki ugomvi, na magomvi yenyewe hata hayama maana ni ya kijinga tu hata aibu kumwambia mtu kuwa hiki ndio cha nzo cha magomvi yetu.

Ikawa kama muujiza tukafanikiwa kutulia kama mwaka nikabeba mimba nyingine nikajifungua mtoto wa 3, tukaanza kulea mtoto mchanga amani tunacheka.

Mara vita ikaanza tukarudi kugombana, hatuelewani mara siku niko kwenye kazi zangu natumiwa sms KUANZIA LEO MIMI SIO MUME WAKO TENA, nataka kumuoa Fulani( huyu dada alikua mchepuko wake) na aliwahi kuwa saabu ya mpasuko wa ndoa yetu kwa sehemu kubwa.


Nikapaniki nikarudi nyumbani nalia kama nimefiwa, basi aliporudi akanambia chukua nguo zako sepa, nikasema siondoki, kipigo nilichopigwa sitasahau nusu anitoe uhai.


Nikaondoka, nikaenda kwa ndugu, akaitwa hakuja, kupigiwa simu akasimamia uamuzi wake kuwa ndio kaamua kuniacha, nikaomba watoto akanipa nikaanza kuishi na watoto peke yetu na hata sijui alipo maana aliamua kuhama na simu kabadili namba.


Baada ya mwaka 1 nikampata mpenzi 3


Maisha ya mapenzi yakaanza penzi likachanua mpaka nikaona angalau dunia ni nzuri penzi likawa tamu, tukapanga mipango ya kuishi wote, na yeye ndio alioanzisha jambo hilo wala sikumwambia kuhusu kuishi wote.


Baada tu ya kukubali kuwa tuanze kuishi wote akaanza kuwa busy hanitafuti iwe kwa simu au sms, ukipiga simu hapokei, sms hajibu, unaweza tuma sms ya kumsalimia asubuhi ikajibiwa usiku, ukipiga simu anaka, au hapokei hata siku 3 na akipokea anakwambia nisubiri kidogo nitakupigia ndio imetoka hadi kesho upige tena, ukimuuliza kama kuna tatizo anajibu hamna, ukimuuliza kama kakuchoka anajibu hapana ila kazi nyingi.


Ukimwambia tuoanane anakubali ikikaribia muda anasema kapata dharura iwe kesho, nk, mwezi sasa yuko ivyo na hatujaonana japo sio mbali. Nimejiongeza kuwa kashaniacha ila kashindwa kusema kuwa kaniacha.


Sasa mapenzi naona niwaachie wengine mimi nipambane na malezi ya wanangu tu.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad