Profesa Mkumbo ataka watu kula bata saa 24




Dodoma. Serikali imeombwa kutazama upya sheria za majiji ili kuruhusu watu kufanya shughuli zao huku wakifurahia kwa masaa yote.

Ombi hilo limetolewa bungeni leo Juni 6, 2022 na Mbunge wa Ubungo, Profesa Kitila Mkumbo wakati akichangia kwenye hotuba ya makadilio ya mapato na matumizi kwa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo kwa bajeti ya mwaka 2022/23.

Profesa Kitila amesema sheria ya iliyopo ambayo inazuia shughuli za biashara za viwnayaji na starehe kwa muda wa asubuhi zimepitwa na wakati hivyo zinapaswa kufumuliwa na kuandaliwa upya.

Amezungumzia suala hilo kwamba limekuwa likiikosesha Serikali mapato ambayo yangekuwa na mchango mkubwa hata kwa uchumi wan chi.


 
Mbunge huyo amesema kuna watu ambao wanafanya kazi za jioni hadi asubuhi kwa hiyo hawana muda wa kufurahi wala kuburudisha miili yao na kwa sheria hiyo inamaana wataendelea kuwa na shida.

Ametolea mfano wa daktari ambaye anasema hivi karibuni alimlalamikia kuwa amekuwa akikamatwa kila wakati anapokunywa bia kabla ya kwenda kazini kwake.

“Yule daktari anafanya kazi katika hospitali moja ya Serikali na kwenye hilo yupo idara ya mochwari, anaingia jioni lakini kabla ya kuingia lazima apate bia sita hivyo akienda kunywa anakamtwa,”amesema Kitila.

Mwananchi
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad