Putin Aibuka Adai Vikwazo Ilivyowekewa Urusi Vinawakabili Wenyewe Walioviweka



Rais wa Urusi Vladimir Putin
RAIS wa Urusi Vladimir Putin amesema anayashangaa Mataifa ya Magharibi kwa kuweka vikwazo ambavyo vinawakabili wao wenyewe na vikwazo hivyo havikuwa na nafasi ya kufanikiwa dhidi ya Urusi tangu mwanzo kabisa.

Putin ameyasema hayo katika kongamano la Kimataifa la Uchumi lililofanyika jijini St Petersburg ambapo amesema Mataifa ya Umoja wa Ulaya yanaweza kupoteza zaidi ya dola Bilioni 400 ambazo ni sawa na Euro Bilioni 326 kutokana na vikwazo vyake dhidi ya Urusi.

Aidha Putin ameongeza kwa kusema kuwa Mataifa hayo yamekuwa yakipambana kutafuta uwiano kati ya vikwazo dhidi ya Urusi na hali yao ya uchumi kwa sasa bila kutegemea ushirikiano wa Urusi.

Achilia mbali ya kauli ya Putin kuhusu uchumi wa Mataifa ya umoja wa Ulaya, Afisa mmoja kutyoka Serikali ya Moscow amethibitisha kuwa vikwazo vilivyowekwa na mataifa ya magharibi vimekuwa na madhara kiasi chake.


 

Bosi wa zamani wa Chelsea raia wa Urusi Roman Abramovich
Gavana wa Benki Kuu Elvira Nabiullina siku ya alhamisi alisema kuwa 15% ya pato la ndani la Taifa (GDP) liliathiriwa na muitikio wa Mataifa ya nje.

“Muitikio kutoka Mataifa ya nje umekuwa mdogo kwa muda mrefu kama siyo jumla kabisa.”Alisema Nabiullina.


Gavana wa Benki Kuu ya Urusi Elvira Nabiullina
Kwa upande mwingine Rais Putin ameendelea kuwasisitiza wawekezaji na wafanyabiashara kuendelea kuwekeza katika nchi yake huku akiwaonya kwa kuwatolea mfano wale aliowashauri kuwekeza nchini humo na wakagoma kumsikiliza ambao kutokana na vikwazo wameambulia kupoteza utajiri wao mkubwa waliokuwa nao na miongoni mwao ni pamoja na tajiri na mmliki wa zamani wa klabu ya Chelsea Roman Abramovich.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad