Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky Afunguka Urusi Kuteka 20% ya Nchi Yake



Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anasema kuwa vikosi vya Urusi vimeteka 20% ya eneo la nchi yake, wakati uvamizi wa Moscow ukikaribia siku kufikia siku 100.

Akiwahutubia wabunge wa Luxembourg, aliongeza kuwa eneo la makabiliano limepanuka na kufikia kilomita zaidi ya kilomita 1,000 (maili 621).

“Makundi yote ya kijeshi ya Urusi yaliyo tayari kupigana yanahusika katika uvamizi huu,” aliwaambia wabunge kupitia kanda ya video.

Vikosi vya Urusi vimekuwa vikizidisha mashambulizi kwenye mji wa Severodonetsk katika eneo la Donbas mashariki.

Maafisa wa ulinzi wa Uingereza wanasema Urusi imeteka sehemu kubwa ya jiji hilo na inapata “mafanikio ya ndani, yanayowezeshwa na mkusanyiko mkubwa wa mizinga”.

Severodonetsk ni mji wa mashariki kabisa chini ya udhibiti wa Ukraine na gavana wa eneo hilo Serhiy Haidai alisema Urusi ilikuwa inajaribu kuvunja ngome ya ulinzi katika mji huo “kutoka pande zote”.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad