Web

Rayvanny "Scene ya Kichoma Gari Kwenye Video Imeniumiza Sana"

Top Post Ad




Mwanamuziki @rayvanny amekiri kuwa katika video ya #Tequiro ambayo ameiachia siku ya leo hakuna scene ambayo imemuumiza kama ile ya kuchoma gari.

Katika wimbo huo ambao amemshirikisha msanii @marioo_tz kuna scene ambayo imeonekana gari aina ya Altezza nyeupe ikiteketea kwa moto katika dakika ya 1:46.




“Najua kweli ni uhalisia lakini yani hakuna scene imeniumiza moyo kama ya kuchoma gari 😭
Director @erismzava naomba tuishie hapa kuchoma vitu” Rayvanny.

Hii ni mara ya pili kwa msanii huyo kuonekana akiteketeza vitu mbalimbali katika video zake ili kutafuta ubora.

Je, tayari umetazama video hio?

Na @blessed_tillah

Below Post Ad

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.